Isaiah 27:1-6

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli

1 aKatika siku ile, Bwana ataadhibu kwa upanga wake,
upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu,
ataadhibu Lewiathani
Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.
yule nyoka apitaye kwa mwendo laini,
Lewiathani yule nyoka mwenye kujipinda;
atamuua joka huyo mkubwa sana wa baharini.

2 cKatika siku ile: “Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:

3 dMimi, Bwana, ninalitunza,
nalinyweshea maji mfululizo.
Ninalichunga usiku na mchana
ili mtu yeyote asije akalidhuru.

4 eMimi sijakasirika.
Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili!
Ningepambana dhidi yake katika vita,
ningeliichoma moto yote.

5 fAu niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,
wao na wafanye amani nami,
naam, wafanye amani nami.”


6 gKatika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi,
Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,
naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.

Copyright information for SwhKC